“Ni lazima tuhakikishe teknolojia inaunga mkono juhudi zetu za kuzuia na kukomesha uhalifu huu, ikiwa ni pamoja na kuongeza ufikiaji na kuwawajibisha watu kwa matendo yao mtandaoni." Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa Siku ya Kimataifa ya 2023   



Kila wimbi jipya la migogoro huongeza ukubwa wa majanga katika Maisha ya mwanadamu.  Unyanyasaji wa kijinsia unaohusiana na migogoro, iwe dhidi ya wanawake, wasichana, wanaume au wavulana katika utofauti wao wote, unaendelea kutumika kama mbinu ya vita, mateso na ugaidi huku kukiwa na kuongezeka kwa migogoro ya kisiasa na kiusalama, ikichangiwa na uvamizi wa kijeshi na kuenea uharamu kwa silaha.  

Migogoro mipya imeongezeka huku migogoro iliyokita mizizi ikiongezeka, na kusababisha kupungua kwa nafasi ya masuala ya kiraia na kuongezeka kwa kisasi dhidi ya watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati, na waandishi wa habari.  Unyanyasaji wa kijinsia na matamshi ya chuki katika unyanyasaji yameongezeka katika ulimwengu wa kidijitali. 

Wakati matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano yamechangia uwezeshaji wa wanawake na wasichana na makundi mengine katika mazingira hatarishi, matumizi yake pia yamewezesha kueneza ukatili.  

Katika baadhi ya mazingira, mienendo ya kutatanisha ya matamshi ya chuki ya kijinsia na vichocheo vya unyanyasaji vilipelekea uwepo wa migogoro ambapo ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia hutumiwa kufedhehesha na kuvuruga jamii zinazolengwa.   

Matamshi ya chuki ikiwa ni pamoja na mtandaoni imekuwa mojawapo ya njia za kawaida za kueneza lugha zinazowagawa watu katika kiwango cha kimataifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post