Kamishna Msaidizi wa Polisi na kamanda wa polisi Mkoani humo ACP Pili Mande akizungumza na vyombo vya habari.

Jeshi la polisi Mkoani Lindi limefanya zoezi la usafi wa mazingira katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi Sokoine ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina yao na wananchi.

Makamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi wakifanya usafi meneo ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi, Sokoine

Zoezi hilo lililofanyika leo limeenda sambamba na utoaji wa msaada kwa akina mama na watoto waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo pamoja na kutoa vifaa vya kufanyia usafi kama fagio kwa ajili ya matumizi ya hospitali. 

Kamishna Msaidizi wa Polisi na kamanda wa polisi Mkoani humo ACP Pili Mande akikabidhi vifaa kwa mama aliyelazwa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi, Sokoine


Kamishna Msaidizi wa Polisi na kamanda wa polisi Mkoani humo ACP Pili Mande aliyeongoza zoezi hilo amesema wameamua kufanya usafi katika eneo la hospitali kuonyesha umuhimu wa usafi kwani watu wengi hufika kwa ajili ya kupata huduma katika maeneo hayo.


Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Lindi Richard Shabani ambaye pia ni afisa afya wa Mkoa huo amesema kitendo cha jeshi la polisi kufanya usafi kama moja ya shughuli  zao, inatoa faraja kwa jamii na kuisaidia sekta ya afya kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na salama.

Post a Comment

Previous Post Next Post